Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MIRADI YA KIMKAKATI BUKOBA KUKAMILIKA KWA WAKATI

MIRADI YA KIMKAKATI BUKOBA KUKAMILIKA KWA WAKATI

 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mkoani Kagera Mhandisi Johnstone Mutasingwa amewahakikishia wananchi wa jimbo hilo kuwa miradi yote ya kimkakati ya maendeleo inayotekelezwa Bukoba mjini itamalizika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa soko kuu, kituo ya mabasi, ujenzi wa barabara kilometa 10 na ujenzi wa kingo za mto Kanoni, Mhandisi Mutasingwa, amesema kuwa mpaka sasa wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo wapo ndani ya muda wa mikataba yao.

“niwahakikishie wananchi ujenzi wa miradi hii upo ndani ya muda kama tunakumbuka utekelezaji wa miradi hii ulianza November mwaka 2025 hivyo bado muda unawaruhusu kufanya utekelezaji ninawaomba wananchi wa Bukoba mjini wawe wavumilivu miradi itakamilika hivi karibuni”

Aidha mbunge huyo amesema kuwa kwa miradi ambayo bado haijaanza kutekelezwa wakandarasi tayari wameishapata vifaa kwajili ya utekelezaji huo, hivyo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika utekelezaji wa miradi hiyo.


“kwa miradi ambayo bado haijaanza utekelezaji wake kama ujenzi wa barabara km 10 inayotekelezwa na kampuni ya Shangdong, ameishakusanya vifaa na anafanya vipimo vya udongo hivyo naamini baada ya mvua kukata miradi hiyo itakamilika na pia nawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali na kuisemea vizuri Bukoba mjini”

Katika hatua nyingine mbunge Mutasingwa amesema kuwa ujenzi wa barabara ya njia nne km 1.6 unatarajiwa kukamilika mwezi wa saba mwaka huu baada ya mkandarasi anayetekeleza mradi huo kupata fedha ya nyongeza ya utekelezaji wa barabara hiyo.

“mkandarasi ameishapata fedha yote ya kukamilisha vipande vyote hivyo ujenzi wa barabara ya njia nne utakamilika hivi karibuni niwahakikishie wananchi kama mvua haitanyesha sana barabara ya njia nne itakamilika mwezi saba”


Sanjali na hayo mwakilishi huyo wa wananchi ameeleza kuwa stendi ndogo ya magari katika ya mji itafunguliwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo la kukatia tiketi, ofisi na jengo la abiria kumpumzikia ambapo kwa sasa amepatikana mkandarasi wa ujenzi wa majengo hayo.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3