MATOEO YA KURA ZA MAONI ISIMANI FREDY VUNJABEI APATA KURA 2,703
TAZAMA FULL VIDEO YA MATOKEO BOFYA LINK HII
Matokeo ya kura za maoni ndani ya chama chama cha Mapinduzi (CCM) yametangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi huo mdogo ndani ya CCM Sule Masanguti,kuwa aliyeongoza ni Fredy Fabian Ngajiro maarufu kama Vunjabei .
Vunjabei ameibuka kinara kwa jumla ya kura 2,703, akifuatiwa Festo Shemu Kiswaga akipata kura 868,huku Emmanuela Kaganda Mtatifikolo akipata kura 682 na Arif Abri kura 233.
Wakati Dkt Abdalah Lusasi kura 100,Claudia Francis (69), Asakwe Widambe (58) Elias Kazikuboma (52), Eng Sebastian Kiyoyo( 37) , Josephat Masambwa (34), David Komba( 27), Tedson Ngwale (24), Egidy Mkolwe (23),Watende Kiyagi (16) , Dkt Tumain Msowoya ( 15), Lazaro Francis Gwira(10), Thitho Cholobi (9), na Thobias Mwilapwa(5).
Matokeo hayo yanaonyesha ushindani mkubwa uliokuwepo katika mchakato huo wa kura za maoni, huku wagombea zaidi ya 15 wakishiriki kuwania nafasi hiyo.
