Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KONAGAMANO LA WANAWAKE KUWAIMARISHA KIUCHUMI KUFANYIKA KESHO MWANZA.

KONAGAMANO LA WANAWAKE KUWAIMARISHA KIUCHUMI KUFANYIKA KESHO MWANZA.


 NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA 

MWANZA, Zaidi ya wanawake 3,000 wanatarajiwa kunufaika na mpango wa “Kafiti na Mwanamke” kupitia uwezeshaji wa mitaji wa biashara ndogo na za kati, upatikanaji wa vifaa vya uzalishaji, mafunzo ya ujasiriamali, pamoja na fursa za masoko na mitandao ya kibiashara.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Kafiti Foundation Mapuli Kafiti ameeleza kuwa Kongamano hilo la wanawake litakalofanyika kesho Aprilini 25. 2026 linalenga kuimarisha uchumi wa wanawake kwa kutoa suluhisho la changamoto zinazowakabili, ikiwemo ukosefu wa mitaji, mifumo rasmi ya kukuza biashara na ulinzi wa kifedha wa muda mrefu.


Mapuli ameeleza kuwa Mpango huo pia utatoa huduma za afya, elimu ya bima na hifadhi ya jamii ili kuhakikisha wanawake wanapata usalama wa kifedha wa sasa na baadaye


ameeleza kuwa Utekelezaji wa mpango huo unafanyika kwa ushirikiano wa CRDB Bank Foundation, NSSF na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, ukilenga kuunganisha huduma za kifedha, ulinzi wa kijamii na utekelezaji wa vitendo.

Meneja wa Kanda ya Ziwa  Benk ya CRDB Denis  Mwoleka ameeleza kuwa  kwa kushirikiana na Kafiti Foundation wanatarajia kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia utoaji wa mitaji mbalimbali zaidi ya shilingi Bilioni 3,kiwango ambacho kinaweza kuwainua wanawake kipato na kuboresha maisha yao pamoja na familia zao.

Mwoleka ameeleza kuwa Mbali na uwezeshaji huo, Kafiti Foundation imekuwa mstari wa mbele katika kutoa fursa kwa vijana na wanawake kupitia mikopo nafuu yenye riba isiyozidi asilimia 7, hali inayowapa nafasi ya kukuza biashara zao bila mzigo mkubwa wa gharama.

"Benki ya CRDB imeendelea kujipambanua kama kinara katika kutoa huduma za kifedha na kusaidia makundi mbalimbali ya jamii, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuchochea maendeleo jumuishi katika sekta tofauti za uchumi" Alisema Mwoleka.


Kwa upande wake Meneja wa NSSF Emmanuel Kahensa ameleza kuwa zaidi ya Wajasiriamali 660 wamewatembelea katika Kata 19 na wamefanikiwa na elimu na kuweza kuwasajili na wanatarajiwa kukabidhiwa kadi zao za uanachama siku ya kesho.


"Zoezi hilo limeenda sambamba na utoaji wa elimu kuhusu skimu ya hifadhi ya mazingira inayolenga kuwainua wajasiriamali wanaojihusisha na shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo, ufugaji, biashara ndogondogo, bodaboda na mama lishe"Alisema

Kahensa amefafanua kuwa Miongoni mwa mafao yanayotolewa na mfuko huo ni pamoja na mafao ya uzee, urithi, ulemavu, matibabu, uzazi pamoja na huduma za mazishi kwa familia ya mwanachama endapo atafariki. Aidha, wanachama wanaweza kuchukua sehemu ya akiba zao kulingana na taratibu zilizowekwa wanapokuwa na uhitaji.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3