Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BBT KOROSHO YAONGEZA HADI KUFIKIA TANI 618000 ZA KOROSHO NCHINI MWAKA HUU WA MAVUNO.

BBT KOROSHO YAONGEZA HADI KUFIKIA TANI 618000 ZA KOROSHO NCHINI MWAKA HUU WA MAVUNO.

 

MATUKIO DAIMA MEDIA.

Utekelezaji wa mpango wa  Jenga kesho iliyobora BBT KOROSHO umeonyesha mafanikio makubwa katika zao la korosho ambapo kwa kitaifa tumeweza kuongeza uzalishaji kutoka tani 528000 ambazo zilikuwa za msimu wa mwaka 2024/25 hadi kufikia tani 618000 katika msimu wa mwaka 2025/26 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 17.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Bodi ya korosho Tanzania tawi la Dar es salaam na Pwani Domina Mkangala wakati akitoa taarifa kwenye Mkutano wa kufanya tathimini ya mpango wa Jenga kesho iliyobora BBT KOROSHO ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa utekelezaji katika mkoa wa Pwani huko wilayani Mkuranga.

Amesema katika mkoa wa Pwani pia tumeona ongezeko la kutoka tani 25000 za korosho katika msimu wa mwaka 2024/25 hadi kufikia tani 35 katika msimu tunaomalizia wa mwaka 25/26 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.

"Niweze kusema kwamba ni kwa mara ya kwanza mkoa wa Pwani tumeweka rekodi kubwa kwa kiwango hicho" alisema Domina.

Aliongeza kuwa "Lakini pia usimalizi madhubuti vya viwatilifu vilivyotolewa kwa ruzuku na uboreshaji wa huduma za Ugani"

Domina alisema serikali inayoongoza na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilijiwekea malengo ya kwamba taifa ifikapo msimu wa mwaka 2029/30 mavuno yafike tani millioni moja ambapo kwa kuwezesha kufanikisha hilo lengo kwa kuongeza na kusogeza huduma za Ugani kwa wakulima wa korosho.

"Na tunatarajia katika msimu wa mwaka 2026/27 kuongeza Maofisa kilimo wa BBT kufikia 812 kwa kuongeza Maofisa Ugani 300 nchi mzima ikiwa katika mkoa wa Pwani tunatarajia kuongeza Maofisa Ugani 30" alisema Domina.

Hatahivyo alisema kupitia mpango huu wa BBT KOROSHO Bodi ya korosho Tanzania imerithia kuwaongezea mkataba wa mwaka mmoja kutokana na utendaji wao wa kazi ambapo kupitia mpango huu wa BBT KOROSHO unalenga kukuza ujuzi kwa wahitimu wa fani za kilimo ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma za Ugani kwa wakulima wa zao la korosho nchini.

Aidha akizungumzia ugawaji wa pembejeo za korosho nchini amesema Ugawaji wa pembejeo katika msimu huu utafanywa na kamati maalumu ya ugawaji wa pembejeo kwa wakulima katika vyama vya msingi AMCOS.

"Na kamati hii itaundwa na Wataalamu kutoka Chama Cha msingi AMCOS husika, Afisa kilimo wa BBT kutoka Bodi ya korosho nchini CBT, Afisa Ugani wa Kata, Mwenyekiti wa Kijiji husika na mtendaji wa Kijiji husika kwa kuzingatia ratiba itakayotolea na Kamati maalumu hiyo itakavyopangwa kwa kuzingatia uzalishaji wao na idadi ya mikorosho waliyonayo ambapo hii itaenda kutusaidia kuthibiti ubadhirifu ulikuwa unatokea katika maeneo mbalimbali na kupunguza malalamiko ya Wakulima katika upatikanaji wa pembejeo"

Awali akifungua Mkutano huo wa tathimini Katibu Tawala wa wilaya ya Mkuranga Omari Mwanga amewataka Maofisa Ugani hao na wao kulima korosho ilikuongeza ufanisi wa usimamizi wa zao hilo la korosho badala ya kuhudumia bila kulima zao hilo la korosho.



Alisema ukiwa Mtaalamu haimaanishi jukumu lao ni kuongoza tu Wakulima Kijijini bali na wao walime zao hilo kwa katika wilaya hiyo bado Kuna maeneo ya kutosha na Ardhi yenye rutuba kwa kuanzisha kilimo hicho ili nawao waweze kujikwamua kiuchumi.

Alisema "Na hii ndio shida tuliyonayo nchini ambapo Wataalamu wanaishia kutufundisha bila wao kuhusika katika mafunzo kwa vitendo kwa dhati wakifanyia jambo hilo lakini mafunzo kwa vitendo yanatija zaidi na watu watahamasika zaidi wakiwaona Wataalamu mkitekeleza kwa vitendo"

+++++++

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3