Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANANCHI BUKOBA WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA KATIKA UNUNUZI NA UUZAJI WA ARIDHI ILI KUEPUKANA NA MIGOGORO YA ARDHI

WANANCHI BUKOBA WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA KATIKA UNUNUZI NA UUZAJI WA ARIDHI ILI KUEPUKANA NA MIGOGORO YA ARDHI

 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Wananchi wilayani Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kufuata taratibu za kisheria wakati wa ununuzi na uuzaji wa ardhi ili kuepukana migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikitokea mara nyingi wilayani humo.

Wito huo huo umetolewa na Afisa Ardhi manispaa ya Bukoba Kurwa  Hanta wakati wa kliniki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi iliyoanzishwa na uongozi wa wilaya ya Bukoba, ambapo amewataka wananchi kufika katika ofisi za manispaa ya Bukoba wakati mtu anahitaji kununua au kuuza ardhi ili kujihakikishia uhalali wa eneo husiku.

“mnapotaka kuuziana ardhi mmeishapatana huko tafadhali fika katika ofisi za mkurugenzi wa manispaa, sisi utakuja kwetu tutajilizisha uhalali wa eneo husika wanaohusiana na mikataba wapo wanasheria wapo mawakili watakusaidia”

Aidha bw.Hanta amewataka wenyeviti wa mitaa manispaa ya Bukoba kuacha kushuhudia mauziano ya ardhi kuepukana na mgangano wa maslai endapo ardhi husika itakuwa na mgogoro.

“wenyeviti wa mitaa kisheria wamekatazwa kushuhudia uuzaji wa ardhi kwa sababu kubwa endapo kutatokea mgogoro mwenyekiti huyo anaweza kulalia upande, lakini pia wenyeviti wa mitaa ndio serikali ya chini kukitokea mgogoro wa aridhi unakuta kuna saini ya mwenyekiti”

Nao baadhi ya wananchi walioudhuria kliniki hiyo akiwemo Bi. Pelagia Joseph, Mkazi wa Bukoba ameshukuru uwepo wa kliniki hiyo na kuwataka viongozi kuwasikiliza wananchi kwa makini na kuzipatia ufumbuzi changamoto zao hasa migogo ya ardhi.

“naomba wendelee kutatua kero za wanachi wawasikilize vizuri kwasababu shida zipo  nyingi mtaani hasa kuhusu ardhi watu wanaangaishwa sana hawapati haki”

Naye Edson Bitesigirwe, Mkazi wa Bukoba amesema kuwa kliniki hiyo itawasaidia watu wengi  kwa sababu wananchi walikuwa na kero nyingi na hawapati msaada na ufumbuzi wa changamoto huko mtaani na katika shughuli zao.

“kliniki hii itawasaidia watu wengi na walika tofauti kwa sababu wananchi wanakero nyingi katika makazi yao na hata kwenye shughuli zao kuna changamoto nyingi”

Kwa upande wake katibu wa CCM manispaa ya Bukoba Shaban Mdoe ametaka wananchi kupatiwa suluhisho na majawabu ya kero zao ili kuondokana na migogoro katika jamii ili wananchi waendelee kuwa na Imani na serikali yao na chama pia.

“kero na changamoto zisikilizwe na majawabu yapatikane tunatamani watu wapate tabasamu na ukisikiliza hapa kero kubwa ni ardhi, ardhi na mimi sijui kwanini haiwezekani kipande cha ardhi kigombaniwe kama watu wanafuata taratibu na sheria za mauziano”

Kliniki hiyo maalum iliyoanzishwa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Yohana Siima itadumu kwa siku nne ikiwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3