Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
VILIO MIILI YA WATUMISHI WA AFYA KIGOMA IKIAGWA

VILIO MIILI YA WATUMISHI WA AFYA KIGOMA IKIAGWA

 

Miili ya watumishi 7 wa halmashauri ya wilaya Kigoma ikiwa katika uwanja wa michezo Kazegunga ambapo iliagwa na viongozi wa serikali,dini, vyama vya siasa na wananchi ili kuruhusu kusafirishwa kwa taratibu za mazishi

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro ameongoza viongozi wa serikali na mamia ya wananchi wa mkoa Kigoma kuwaaga watumishi wa halmashauri ya wilaya Kigoma waliofariki kwa kuzama na boti ziwa Tanganyika juzi huku Rais Samia Suluhu Hassan akitangaza kugharamia taratibu za mazishi na pole kwa wafiwa sambamba na  matibabu na pole kwa majeruhiumla

Jumla ya miili saba iliagwa jana na kukabidhiwa kwa ndugu zao tayari kwa taratibu za safari na mazishi ambapo kati ya miili saba iliyoagwa jana miili mitanno imesafirishwa kwenda mikoa mbalimbali ya Tanzania huku wqaumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Kigoma wakiongoza safari za miili hiyo.


Akizungumza wakati wa kuaga miili hiyo Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro  alisema kuwa marehemu wanaagwa wakiwa mashujaa kwani wamekufa wakiwa katika kutekeleza majukumu ya Kitaifa na kwamba ni simanzi kubwa kupoteza idadi kubwa ya watumishi wengi kiasi hicho wengi wakiwa ndiyo wanaanza taratibu za utumishi.

Balozi Sirro alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amechukua jukumu lote la a kugharamia masanduku ya kusafirishia miili hiyo pia rambi rambi ya Shilingi milioni moja kwa kila mwili na shilingi 200,000 kwa kila majeruhi na kwamba gharama za matibabu zote zitalipwa na serikali hata ikilazimika kupata rufa kwenye hospitali kubwa nchini.


Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Kiza Mayeye alisema kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa na msiba wa watumishi hao ambao walikuwa wanachangia kupunguza changamoto kubwa ya watumishi ambaayo ilikuwa inaikabili halmashauri hiyo ambapo ametoa pole kwa familia za marehemu, halmashauri ya wilaya Kigoma, Mkuu wa mkoa Kigoma na watu wote walioguswa moja kwa moja na msiba huo na kwamba mapenzi ya Mungu yametimizwa.

Akizungumza katika kuaga miili hiyo, kurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kigoma, Chiriku, Chilumba alisema kuwa Halmashauri imesimamia taratibu zote za mazishi ya marehemu hao kwa mujibu wa taratibu za stahiki za utumishi na maelekezo ya viongozi wa mkoa na Kitaifa na miili yote utasafirishwa kwenda maeneo yambayo familia zimetangaza mazishi yateenda kufanyika.

Aidha Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI,Dk.Paul Chaote amesemaa kuwa wizara imepokea taarifa hiyo kwa majonzi makubwa na kwamba wanaunga na familia kuwatakia punguzo mema wote waliofariki lakini pia kuwatakia uponyaji wa haraka ya majeruuhi.

Miili ya watumishi walioagwa ni pamoja na Erick Dabanga (27), Jofrey Aron (26), Rachael Msalila (29),Winny Bayabusani (32), .Joyce Kandole (31), Paul Luvanda (31) na Omari Karim (29) ambapo hadi sasa mwili wa Amos Joel Sika haujapatikana.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3