UJENZI WA SOKO LA MROMBO UATEMBELEWA NA KAMATI YA KUDUMI YA BUNGE TAMISEMI.
Na,Jusline Marco:Arusha
Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI imetembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa soko la Mrombo lililopo jijini Arusha ambapo wajumbe hao wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, mradi ambao unakwenda kuimarisha mazingira bora ya wafanyabiashara wadogo na kuboresha hali ya usafi kwenye bidhaa wa za wajasiriamali hayo kwa kuzingatia afya ya mlaji.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Florent Kyombo amepongeza Serilali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa wafanyabiashara ndogo na kuwajenga soko la kisasa, soko ambalo litaboresha mazingira ya wafanyabiashara hawa na kuhakikisha usalama wa wafanyabiashara na wateja wao.
Aidha wameipongeza Serikali chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri inayoendelea katika jiji la Arusha na kushauri kuendelea kusimamia mkandarasi aongeze kasi ili muda wa miezi 6 alioongezewa Mkandarasi uwe wa mwisho na mradi ukamilike kwa muda huo.
Sambamba na hayo amewapongeza viongozi wa ngazi zote kuanzia Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, mkoa, wilaya na halmashauri na timu ya watendaji wa ngazi zote pamoja na wafanyabiashara waliokubali kupisha maeneo hayo pamoja na wananchi ambao hawako nyuma kuhakikisha mradi huo unaendelea vizuri wakati wote wa utekelezaji wake.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo amesema mradi huo unatekelezwa na Serikali kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.2 na unatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya CBS Consultant Ltd ya Jijini Dar es salaam.


.jpeg)
