Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SERIKALI YAENDELEA KUTENGA MAENEO NA KUTOA LESENI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

SERIKALI YAENDELEA KUTENGA MAENEO NA KUTOA LESENI KWA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma


MKURUGENZI wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini, Hamisi Kamando, amesema serikali inaendelea kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini, kuwapatia leseni na kuwaendeleza ili waweze kunufaika na rasilimali za madini.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Mhandisi Kamando amesema kuwa kupitia Wizara ya Madini, serikali imeendelea kutenga maeneo ya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo nchini, ambapo hadi sasa jumla ya maeneo 65 yamependekezwa kutengwa kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi.


Amesema maeneo hayo yapo katika mikoa mbalimbali ya kimadini ikiwemo Mtwara, Manyara, Lindi, Morogoro, Dodoma, Tabora, Pwani, Tanga, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Mbeya na Ruvuma.


Aidha amesema katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2025, serikali ilitoa jumla ya leseni 5,983 za uchimbaji mdogo wa madini, sawa na asilimia 71 ya leseni zote zilizotolewa katika kipindi hicho, ambapo leseni hizo hutolewa kwa Watanzania pekee na sehemu kubwa ya waombaji ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 45.


Pia alieleza kuwa kupitia mradi wa Mining for Better Tomorrow (MBT), Tume ya Madini imetoa leseni 273 kwa vikundi 183 vya vijana vilivyosajiliwa kwenye halmashauri katika mikoa mbalimbali ya kimadini.


" Leseni hizi zinahusisha uchimbaji wa madini ya dhahabu, shaba, madini ya vito, madini ya viwandani kama chumvi pamoja na madini ya ujenzi.


Na kuongeza "Hadi kufikia Desemba 2025 mradi huo umewezesha vijana 2,550 kupata ajira za moja kwa moja, hatua inayosaidia kuongeza ushiriki wa vijana katika sekta ya madini na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi,"amesema amesema Mhandisi Kamando.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3