Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
RAIS TRUMP ATAKA IRAN KUJISAMILISHA BILA MASHARTI

RAIS TRUMP ATAKA IRAN KUJISAMILISHA BILA MASHARTI

 


Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakutakuwa na makubaliano yoyote kati ya nchi yake na Iran, isipokuwa taifa hilo lijisalimishe bila masharti, akisisitiza kuwa hatua hiyo ndiyo pekee inayoweza kumaliza mzozo unaoendelea katika Mashariki ya Kati. 

Kauli hiyo imekuja wakati mvutano wa kijeshi kati ya Marekani, Israel na Iran ukiendelea kuongezeka, huku Trump akisisitiza hakuna nafasi ya mazungumzo ya kawaida hadi Iran ikubali kujisalimisha.

 Katika hatua nyingine ya kidiplomasia, Rais wa Russia, Vladimir Putin amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kiongozi wa Iran, akitoa pole kwa vifo vilivyotokea kutokana na mapigano hayo.

 Putin amesisitiza umuhimu wa kutafuta suluhisho la kidiplomasia ili kupunguza mvutano na kuzuia kuongezeka kwa machafuko katika ukanda huo.

 Mvutano huo umeendelea kuvuta hisia za jumuiya ya kimataifa, huku baadhi ya nchi na taasisi za kimataifa zikitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na kuanza mazungumzo ya amani kuepusha athari kubwa zaidi kwa usalama wa dunia na uchumi wa kimataifa. Endelea kufuatilia Mwananchi


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3