MWANADIPLOMASIA MWENYE MIAKA 93 KUSHTAKIWA KWA MAUAJI YA PATRICE LUMUMBA
Mar 17, 2026
Mwanadiplomasia wa zamani wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 93 ameamriwa kufikishwa mahakamani katika kesi ya mauaji ya mwanaharakati wa uhuru wa Kongo Patrice Lumumba mwaka wa 1961. Uamuzi huo wa mahakama umesifiwa kama hatua kubwa kuelekea kukabiliana na historia ya ukoloni ya nchi hiyo.
Etienne Davignon, ambaye aliwahi kuwa kamishna wa Ulaya na mtu pekee ambaye bado yuko hai kati ya Wabelgiji 10 wanaoshutumiwa na familia ya kiongozi huyo wa Kongo kwa kushiriki katika mauaji yake, anashtakiwa kwa kushiriki katika "uhalifu wa kivita".
Mjukuu wa waziri mkuu huyo wa zamani, Mehdi Lumumba, ameukaribisha uamuzi wa mahakama ya Brussels -- ambao bado unaweza kukatiwa rufaa akiuita "wa kihistoria."
Ikiwa kesi hiyo itaendelea, Davignon atakuwa afisa wa kwanza wa Ubelgiji kushitakiwa katika kipindi cha miaka 65 tangu Lumumba kunyongwa na mwili wake kuyeyushwa katika tindikali.

.jpg)
