Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MHE. KOOLA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ASHIRIKI MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR’AN - HIMO*

MHE. KOOLA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ASHIRIKI MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR’AN - HIMO*



Jana, tarehe 28 februari 2026. 

Mbunge wa Jimbo la Vunjo, *Mhe. Enock Koola,* alishiriki kama Mgeni Rasmi katika Madhimisho ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur’an yaliyofanyika Mji Mdogo wa Himo, Jimbo la Vunjo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Koola alisema;

"Nawapongeza sana walimu wa madrasa kwa juhudi zao za malezi ya kiroho na maadili kwa watoto na vijana kupitia elimu ya dini. Pia, niwapongeze washiriki wote kwa nidhamu, juhudi na kujituma katika mashindano hayo muhimu kwa ustawi wa jamii." 

Mheshimiwa Mbunge aliwahimiza vijana kuendelea kushikamana na misingi ya imani, kuzingatia masomo yao darasani pamoja na kuepuka makundi yenye mienendo hatarishi ili kujenga jamii salama na Taifa lenye kizazi chenye maadili mema.

Katika kuhitimisha hafla hiyo, Mheshimiwa Koola alikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano, vyeti kwa washiriki wote, pamoja na zawadi maalum kwa walimu na majaji waliowezesha kufanikisha mashindano hayo.

*Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Vunjo*




 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3