KIHONGOSI KUTATUA KERO ZA WANANCHI KAGERA
Msemaji na Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa chama cha mapinduzi CCM taifa Kenani Kiongosi anatarajiwa kufanya ziara mkoani Kagera kuanzia march 26 hadi 28 mwaka huu kwa lengo la kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa Imani ya chama hicho.
Akizunguama na waandishi wa habari katibu wa siasa uenezi na mafunzo mkoa wa Kagera wa CCM, Hamim Mahmoud amesema kuwa lengo la ujio wa Kihongosi ni kuimarisha chama kwa kwenda kwenye mashina ya chama, kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia utekelezaji wa Imani ya chama.
"lengo ni kuimarisha chama kwa kutembelea mashina na kuongea na mabalozi wa mashina na wanachama, kutembelea miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa ipasavyo"
Aidha amesema kuwa katika ziara ya kiongozi huyo atafanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero na changamoto za wananchi na kuzipatia ufumbuzi papo hapo ili kuhakikisha wananchi wataendelea kuwa na imani na CCM na serikali yao.
"na mada pendwa kupitia mikutano ya hadhara ni kusikiliza kero na dukuduku zao na kuzipatia ufumbuzi papo hapo kwani atakuwa na wataalamu wa idara zote ndani ya mkoa na hata wa nje atapigiwa simu ili kuhakikisha ufumbuzi wa changamoto za wananchi unapatikana"
Sanjali na hayo Hamim amewaomba wananchi wenye changamoto na kero mbalimbali kujitokeza kwa wingi na pia kujitokeza katika mikutano ya hadhara kusikiliza msemaji huyo wa CCM taifa.
"niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya hadhara atakayo ifanya katika maeneo yao ikiwemo mkutano mkubwa wa hadhara atakaoufanya katika viwanja vya Uhuru platform (Mayunga) manispaa ya Bukoba siku ya tarehe 26 March.
Akiwa mkoani Kagera Kenani Kihongosi anatarajiwa kutembelea wilaya tatu za Bukoba March 26, Muleba March 27 na Biharamulo March 28.


