Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
USHIRIKIANO WA POLISI NA TANESCO WAIMARISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

USHIRIKIANO WA POLISI NA TANESCO WAIMARISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi Grace Ntungi, amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa juhudi zake za kutokomeza vitendo vya uhalifu pamoja na kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.


Pongezi hizo zimetolewa Februari 11, 2026 wakati Mhandisi Ntungi alipotembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kwa lengo la kukabidhi jiko janja litakalosaidia kuendeleza matumizi ya nishati safi na rafiki kwa mazingira ndani ya taasisi hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhandisi Ntungi alisema ushirikiano kati ya TANESCO na Jeshi la Polisi ni muhimu si tu katika masuala ya usalama wa miundombinu ya umeme, bali pia katika kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya nishati mbadala na teknolojia rafiki kwa mazingira.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amelishukuru Shirika la TANESCO kwa pongezi hizo pamoja na zawadi ya jiko janja, akisema kuwa hatua hiyo ni ishara ya umoja, upendo na mshikamano uliopo kati ya taasisi hizo mbili.

SACP Bukumbi aliongeza kuwa ushirikiano huo unaongeza ari ya kufanya kazi kwa pamoja katika kuhudumia jamii, kulinda rasilimali za taifa pamoja na kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3