Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
TAKUKURU YASIMAMIA THAMANI YA FEDHA MIRADI YA BILIONI 7.1

TAKUKURU YASIMAMIA THAMANI YA FEDHA MIRADI YA BILIONI 7.1


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa Kigoma imefanikiwa kusimamia thamani ya fedha kwenye miradi 27 yenye thamani ya shilingi Bilioni 7.1 ambapo baadhi ya miradi ilikiuka mikataba kwa kubadilisha michoro ya majengo na kununua vifaa ambavyo havikuwa na ubora.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa Kigoma, Asha Kwariko akitoa taarifa ya utendaji wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Desemba 2025 alisema kuwa Katika hilo Mkuu huyo wa TAKUKURU alisema kuwa kutokana na hilo taasisi hiyo ilifanikisha kurudiwa kwa baadhi ya miradi hiyo na kununuliwa kwa vifaa vilivyopo kwenye mkataba tofauti na vilivyokuwa vimewekwa.

Kwariko alisema kuwa katika miradi hiyo 27 jumla ya miradi 22 ya elimu ilifanyiwa ukaguzi ambapo ilibainika kuwa baadhi ya majengo ya madarasa yamejengwa kinyume na ramani ya wizara ya elimu, na baadhi ya vifaa vilivuonunuliwa vilikuwa na ubora wa chini na  kutokuwepo kwa nyaraka za malipo ya wazabuni, ujenzi kutofuata mkataba wa ujenzi (BoQ)

Kutokaba na hali hiyo alisema kuwa Wakandarasi wa ujenzi walitakiwa kurudia miradi na kufuata maelekezo yaliyopo kwenye BoQ sambamba na wasimamizi wa miradi hiyo kusimamia maelelezo yaliyopo.

Katika hatUa nyingine taasisi hiyo imesema kuwa mpango wa taasisi hiyo wa kusikiliza kero za wananchi maarufu kama TAKUKURU RAFIKI imefanikisha ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kabare wilaya ya Kakonko  mkoani Kigoma iliyojengwa na Shirika la World Vision kwa gharama ya shilingi Milioni 246.

wananchi wa kijiji hicho hawakuwa na zahanati hivyo wakati wa Program ya TAKUKURU Rafiki wananchi hao walitoa malalamiko ya adha kubwa wanayopata kwa kutokuwa na zahanati hivyo kufuata huduma za afya umbali mrefu



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3