Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SIRRO ATAKA MIRADI YA BARABARA KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA DIRA YA TAIFA

SIRRO ATAKA MIRADI YA BARABARA KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA DIRA YA TAIFA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amezitaka wakala wa barabara (TANROADS) na Wakala wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA) kuekeleza majukumu yao ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa kuzingatia mpango wa maendeleo ya Taifa na vipaumbele vya hali halisi ya mkoa Kigoma,

Balozi Sirro alisema hayo akizungumza kikao cha bodi ya barabara mkoa Kigoma na kubainisha kuwa mpango wa maendeleo ya Taifa umeanisha kila jambo ambalo linapaswa kufanywa na taasisi na mamlaka mbalimbali za serikali na wadau wake akitaka pia vipaumbele viwekwe kwenye utekelelzaji wa miradi  ya miradi ya barabara ngazi ya mkoa.

Katika kikao hicho Mkuu huyo wa mkoa alizitaka mamlaka hizo za barabara kuweka kipaumbele katika utekelezaji wa barabara za mkoa huo kuendana na mpango wa serikali wa kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkakati kiuchumi na biashara kwa ajili ya nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Aidha Balozi Sirro amezitaka TARURA na TANROADS kuongeza ubunifu katika kutafuta suluhu endelevu ya miradi ya barabara ikiwemo kuongeza matumizi ya teknolojia na gharama nafuu za miradi yaa barabara huku akitaka pia kufanyika ukaguzi wa mara kwa mara wa barabara za mkoa huo.

Akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini, Profesa Joyce Ndalichako alipongeza utekelezaji wa miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA na TANROADS lakini amebainisha kuwa bado hakuna barabara saidizi (Access Roads) wala michepuko ya barabara kuelekea maeneo ya utoaji huduma za kijamii kutoka barabara kuu.

Akizungumza katika kikao hicho Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Kiza Mayeye alisema kuwa bado ujenzi wa barabara ya Mwandiga kuelekea Kagunga una kasi ndogo hivyo kuitaka TANROADS kuongeza kasi lakini kueleza uhalisi wa wapi changamoto ilipo ili waweze kusaidia kwenye mamlaka za juu za serikali 




 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3