MTOTO WA MUAMMAR GADDAFI AUAWA LIBYA
Feb 3, 2026
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
MTOTO wa aliyekuwa Rais wa Libya, Hayati Muammar Gaddafi, Saif al-Islam ameripotiwa kuuawa katika eneo la Zintan nchini Libya, hiyo ni kwa mujibu wa wakili wake, ambapo tukio hilo limeripotiwa bila kutoa maelezo kuhusu sababu au mazingira ya kifo chake.
Seif al-Islam Gaddafi alipendekezwa kuwa Mrithi wa baba yake Muammar Gaddafi. Mnamo 2021, aliwasilisha ombi lake kugombea Urais.
Seif mwenye umri wa miaka 53 alikuwa akisakwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, kesi ambayo Mawakili wake hawakuweza kuitupilia mbali.

