Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KILIO CHA MWANAFUNZI CHAWAFIKIA SERIKALI HATUA

KILIO CHA MWANAFUNZI CHAWAFIKIA SERIKALI HATUA



Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

SERIKALI imeingilia kati malalamiko ya wanafunzi wanaotumia usafiri wa mabasi ya mijini maarufu kama daladala baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Jangwani Mariana Eric Mirindima akiwasilisha barua iliyoeleza changamoto kubwa wanazokutana nazo wanafunzi wanapotumia usafiri huo. 

Katika video hiyo mwanafunzi huyo alieleza kuwa makondakta wamekuwa wakigoma kuwabeba wanafunzi wakidai hawalipi nauli kamili hali inayowalazimu wanafunzi kusimama barabarani kwa muda mrefu kuchelewa kufika shuleni au kushindwa kabisa kuhudhuria masomo hali ambayo inaathiri elimu usalama na ustawi wao. 

Akizungumza na waandishi wa habari Bungeni Dodoma kuhusu suala hilo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa amesema Serikali imesikiliza kilio cha mwanafunzi huyo na wanafunzi wengine na kusisitiza kuwa sauti yao itafanyiwa kazi kwa vitendo Waziri Makame Mbarawa amempongeza mwanafunzi Mariana pamoja na mzazi wake kwa ujasiri wa kupaza sauti na kutoa mrejesho unaosaidia Serikali kuboresha huduma za kijamii

" Kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA Serikali itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya madereva na makondakta wote wanaokiuka sheria na kuwanyanyasa wanafunzi huku akieleza kuwa tayari Serikali imeweka mikakati ya kuboresha usafiri wa wanafunzi ikiwemo uendeshaji wa mabasi maalumu ya wanafunzi nyakati za asubuhi na jioni utengaji wa mabehewa maalumu kwenye treni za mijini pamoja na kurasimisha nauli ya shilingi mia mbili kwa wanafunzi, " Amesema. 

Aidha Waziri Makame Mbarawa ameielekeza LATRA kuimarisha udhibiti wa nauli staha ya huduma na usalama wa wanafunzi kuhakikisha mabasi na treni zote zina namba za bure za kutoa taarifa kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi wa kushtukiza hasa nyakati za kwenda na kurudi shule na kuendelea kutoa elimu kwa watoa huduma na abiria kuhusu haki na wajibu wao. 

Serikali pia imewataka wananchi kushirikiana kuwatetea wanafunzi pale wanaponyanyaswa kwa kutoa ushahidi kwa mamlaka husika huku ikiwatahadharisha wamiliki wa daladala kuhakikisha watumishi wao wanazingatia sheria na kanuni za usafiri lengo likiwa ni kujenga mfumo wa usafiri wa umma unaolinda haki usalama na ustawi wa wanafunzi na wananchi wote nchini.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3