Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BOT YAKEMEA TABIA YA KUHARIBU NOTI KWA MAPAMBO YA VELENTINE

BOT YAKEMEA TABIA YA KUHARIBU NOTI KWA MAPAMBO YA VELENTINE



Matukio Daima Media ,Dodoma .

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeibuka na kukemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi kutumia fedha kama mapambo ya Valentine, ikisema kitendo hicho kinaigharimu nchi mabilioni ya shilingi.

Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, amesema noti zinazotumika kufungwa kwenye mashada ya maua huharibika haraka na kushindwa kuendelea kutumika kwenye mzunguko wa fedha.

Amesema mara nyingi fedha hizo hubandikwa gundi na kukunjwa, hali inayozifanya zipasuke, zichanike au kupoteza ubora wake.

“Hizi fedha ni mali ya Watanzania wote. Zinapoharibiwa, mzigo unaangukia Serikali na wananchi kwa ujumla,” amesema.

BoT imewataka wananchi kuacha mara moja tabia hiyo na kutumia njia mbadala za kuonyesha mapenzi bila kuharibu mali ya Taifa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3