Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA VITUO VYA KUSUKUMA NA KUHIFADHI MAJI MWANZA

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA VITUO VYA KUSUKUMA NA KUHIFADHI MAJI MWANZA


NA CHAUSIKU SAID 
MATUKIO DAIMA MWANZA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa vituo vya kusukuma maji,mabomba makuu ya kusafisha maji na matenki ya kuhifadhi maji utakaogharimu kiasi Cha Sh Bilioni 46  katika mtaa wa Sahwa kata ya Lwahnima wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.


Mradi huo unaotekelezwa chini ya programu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Ziwa Victoria (LVWATSAN) umewekewa jiwe la msingi leo January 23, 2026.



Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi Dkt. Nchimbi amewasihi wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kufanya kazi kwa bidii ili uweze kukamilika kwa wakati hatua itakayosaidia wananchi kuondokana na kero ya maji.


"Serikali ya awamu ya sita inaendelea kukamilisha miradi mbalimbali katika mkoa wa mwanza ikiwemo ya maji hivyo wakandarasi wanapaswa kufanya kazi usiku na mchana ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa haraka na kuleta tija kwa wananchi", Amesema Dkt. Nchemba


Kwaupande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (MWAUWASA), Nelly Msuya amesema mradi huo unagharimu zaidi ya bilioni 46 na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 450,000 walioko katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa mwanza.



Aidha, ameeleza kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa Juni 2024 na unatarajia kukamilika Desemba mwaka huu.






Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3