KATIBU CHADEMA RUNGWE ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI.
Jan 30, 2026
Polisi Mkoa wa Mbeya imemkamata Award Karonga, Mkazi wa Katumba wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambaye ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Rungwe akituhumiwa kwa makosa ya kichochezi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Benjamin Kuzaga, kupitia taarifa yake kwa umma, amesema mtuhumiwa alikamatwa Januari 29, 2026 saa 4 asubuhi katika eneo la Katumba, Kata ya Ibighi Tukuyu Wilaya ya Rungwe kwa tuhuma mbalimbali za kijinai ikiwepo uchochezi.

