Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BAADA YA MIAKA 40 BAHARINI ,MABAHARIA WAZAMIA UTALII WA NDANI MIKUMI BA SGR

BAADA YA MIAKA 40 BAHARINI ,MABAHARIA WAZAMIA UTALII WA NDANI MIKUMI BA SGR

Na atukio Daima Media Morogoro

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabaharia Wazoefu Tanzania, Juma Simba Ghadafi, amesema Watanzania wanapaswa kuunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali katika kuendeleza na kutangaza utalii wa ndani, akisema sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa.


Akizungumza wakati wa ziara ya mabaharia hao katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Ghadafi alisema ziara hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuitangaza nchi kimataifa kupitia filamu ya Royal Tour, sambamba na uwekezaji mkubwa unaoendelea katika miundombinu.

Alisema mabaharia wazoefu, licha ya kutumia muda mwingi nje ya nchi kutokana na kazi zao za baharini, bado wana wajibu wa kuipenda, kuijali na kuithamini Tanzania kwa kutembelea vivutio vya ndani na kuhamasisha wengine kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya ya Mabaharia Wazoefu Tanzania, Danny Masele, alisema usafiri wa treni ya SGR waliotumia mabaharia takribani 20 kufika Morogoro na hatimaye Mikumi umeleta mapinduzi makubwa kwa Watanzania, akibainisha kuwa safari yao hadi Mikumi imekuwa ya haraka, salama na yenye faraja.


Aliongeza kuwa SGR imefungua fursa mpya za utalii kwa wananchi wa kawaida, kwani imepunguza gharama na muda wa kusafiri kwenda kwenye hifadhi na vivutio mbalimbali.

Baharia Shahibu Ngota alisema uwepo wa miundombinu ya kisasa umeongeza hamasa ya kutembelea hifadhi, akisema safari yao kwa SGR imewapa uzoefu mzuri na kuwafanya wajivunie maendeleo yaliyofikiwa.

Naye Baharia Mohammed Jagga aliwahimiza mabaharia waliolowea nje ya nchi kurejea nyumbani, akisema Tanzania kwa sasa ina mazingira mazuri ya kuishi na kuwekeza kutokana na amani, utulivu na miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa.


Alisema kurejea kwa wazawa walioko nje kutasaidia kuhamisha ujuzi na uzoefu walioupata duniani na kuuchangia katika maendeleo ya taifa.

Akawataka mabaharia walio kazini, kutumia fursa ya kuzunguka maeneo mbalimbali duniani kuwa mabalozi wa Tanzania kwenye kila nchi watakayofika.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3