Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
AANZA SAFARI YA MIKOA 31 KWA BAISKELI KUHAMASISHA UHIFADHI MAZINGIRA

AANZA SAFARI YA MIKOA 31 KWA BAISKELI KUHAMASISHA UHIFADHI MAZINGIRA

 

Mkuu wa wilaya Kasulu Kanali Athana Murimi (kulia)  akikabidhi bendera ya halmashauri ya mji  Kasulu kwa Mwalimu Wenseslaus Lugaya ambaye ameanza safari ya kutembea kwa baiskeli mikoa 31 kuhamasisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

          Mwalimu Wenseslaus Justine Lugaya Mwalim wa shule ya Msingi katika halmashauri ya mji  wa Kasulu ameanza safari ya kilometa 8721 kutembea kwa baiskeli akitembelea mikoa 31 ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa  lengo la kuhamasisha uhifadhi na utunzaji wa mazingira.


Akizungumza katika hafla ya kumuaga mbele ya Mkuu wa wilaya Kasulu, Kanali Athanas Murimi 16 Novemba  mwaka huu   Mjini Kasulu Mwalim Lugaya alisema kuwa katika safari yake atatembelea mikoa 26 ya Tanzania Bara na mitano ya Zanzibar kwa umbali wa kilomita 8,721 na Kamba  safari hiyo itakamilika tarehe 16 Februari 2027.


Mwalim Lugaya alisema kuwa safari ina  lengo la kuhamasisha upandaji wa miti  milioni 1.5  ikiwa imebeba ujumbe wa kuwataka Watanzania  kuzingatia upandaji miti na utunzaji wa mazingira kuchukua hatua za vitendo katika kulinda mazingira na kujenga mustakabali endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.


kauli mbiu ya safari hiyo ikiwa  inasema “Tunza Mazingira, Dumisha Muungano, Tekeleza Dira Taifa 2050.” 


Akikabidhi bendera ya Halmashauri ya Mji Kasulu ambapo Mwalimu huyo anafanya kazi Mkuu wa wilaya Kasulu, Athanas Murimi alisema kuwa athari za mabadilko ya Tabia nchi yanamuathiri kila Mtanzania hivyo ametaka watu wote kumuunga mkono mwendesha baiskeli hiyo kwa kujitolea kufanya kazi kubwa na y a kutukuka kwa ajili ya Watanzania.


Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3