Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAZIRI WA ULINZI NA JKT AWATEMBELEA NA KUWAJULIA HALI WAKUU WA MAJESHI WASTAAFU

WAZIRI WA ULINZI NA JKT AWATEMBELEA NA KUWAJULIA HALI WAKUU WA MAJESHI WASTAAFU

 



Na Matukio Daima Media

 

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 27 Oktoba 2026, amewatembelea na kuwajulia hali Wakuu wa Majeshi Wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Robert Mboma na Jenerali Davies Mwamunyange, katika makazi yao yaliyopo Mbweni na Tangi Bovu, jijini Dar es Salaam.


Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za Waziri wa Ulinzi na JKT za kuwatembelea, kuwajulia hali na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wastaafu wa JWTZ, ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wao katika kulitumikia Taifa na kulijenga Jeshi la Wananchi wa Tanzania.


Kupitia ziara hizo, Waziri wa Ulinzi na JKT, anaendelea kudumisha mawasiliano na viongozi hao wastaafu, ambao wana uzoefu mkubwa na historia muhimu katika uongozi na maendeleo ya Jeshi.








Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3