Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
TOSCI YAIMARISHA UDHIBITI WA MBEGU BORA KWA KUKABIDHI GARI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

TOSCI YAIMARISHA UDHIBITI WA MBEGU BORA KWA KUKABIDHI GARI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI


Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imeimarisha utekelezaji wa shughuli za udhibiti wa ubora wa mbegu katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa kukabidhi gari aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop, litakalorahisisha usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za ukaguzi wa mbegu katika maeneo mbalimbali ya kanda hiyo.


Gari hilo limekabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TOSCI, Bi. Lilian Schechambo, kwa Kaimu Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Frank Mwilenga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.

Upatikanaji wa gari hilo unatarajiwa kurahisisha safari za kikazi kwa wataalamu wa TOSCI, hususan katika kufuatilia shughuli za uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mbegu, pamoja na kukagua ubora wa mbegu zinazowafikia wakulima.

Udhibiti madhubuti wa ubora wa mbegu ni hatua muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata mbegu zinazokidhi viwango vinavyotakiwa, jambo linalochangia kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao na kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Hatua hiyo inaonesha umuhimu wa kuimarisha rasilimali za kiutendaji kwa taasisi zinazohusika na udhibiti wa ubora wa pembejeo za kilimo, ili kuhakikisha wakulima wanapata huduma bora na mbegu zinazoweza kuwasaidia kuongeza uzalishaji na kipato.



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3