Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI REKEBISHI WA TITI KWA MARA YA KWANZA TANZANIA KWA TEKNOLOJIA YA HADUBINI

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI REKEBISHI WA TITI KWA MARA YA KWANZA TANZANIA KWA TEKNOLOJIA YA HADUBINI


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kufanya kwa mara ya kwanza nchini Tanzania upasuaji rekebishi wa titi kwa kutumia hadubini, kwa mbinu yakutumia mbinu ya Deep Inferior Epigastric Perforator (DIEP flap), inayohusisha kuhamisha tishu kutoka sehemu ya tumbo kwenda kwenye titi, huku mishipa yake ya damu ikiunganishwa na mishipa ya damu ya eneo jipya ili kuboresha mwonekano wa titi.


 Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano kati ya wataalamu wa Muhimbili na jopo la madaktari bingwa 10 kutoka Marekani, waliotembelea hospitali hiyo kwa ajili ya kubadilishana ujuzi na uzoefu katika upasuaji rekebishi na matumizi ya teknolojia za kisasa za matibabu.

Katika ushirikiano huo, wagonjwa wanne wamefanikiwa kufanyiwa upasuaji rekebishi na wanaendelea vizuri baada ya matibabu hatua inayoonesha uwezo wa Muhimbili katika kuendeleza huduma za upasuaji wa kibingwa, kutumia mbinu za kisasa na kuongeza ujuzi wa wataalamu wake kupitia ushirikiano wa kimataifa, kwa lengo la kuboresha matokeo ya matibabu na huduma kwa wagonjwa nchini.


 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3