Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MKANDARASI MRADI WA UMEME MALAGARASI APEWA TAHADHARI YA EL NINO

MKANDARASI MRADI WA UMEME MALAGARASI APEWA TAHADHARI YA EL NINO


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

SERIKALI mkoani Kigoma imemtahadharisha Mkandarasi anayetekeleza mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwenye eneo la Igamba Mto Malagarasi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa za El Nino ambazo zimeanza kunyesha ili mvua hizo zisivuruge utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 430.
 
Katibu Tawala wa mkkoa Kigoma,Hassan Rugwa alisema hayo alipotembelea mradi huo na kuzungumza na Mkandarasi wa mradi huo Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation (DEC) na wasimamizi wa mradi huo kutoka Shirika la uzalishaji na usambazaji umeme nchini (TANESCO) akieleza kuridhiswha na hatua ya sasa ya maendeleo ya mradi huo.
 
Rugwa alisema kuwa mradi huo wenye thamani ya ni muhimu kwa maendeleo ya mkoa Kigoma na nchi kwa jumla hivyo ni lazima serikali ihakikishe inasimamia kwa karibu kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unafanyika kulingana na mkataba uliopo hivyo wkandarasi na wasimamizi wa mradi wanapaswa kuchukua tahadhari zote ili mradi usikwame.
  
Awali Msimamizi wa mradi huo Majuba Mzungu kutoka TANESCO alisema kuwa mradi huo ambao una miradi mitatu ndani yake unatekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 430 ukitarajia kutoa Mega Watt 49.5 ambapo kwa mradi utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 31.7 na mradi unatarajia kukamilika
 
Mzungu alisema kuwa pamoja na uzalishaji wa umeme Mega Watt 49.5 pia mradi huo una mradi wa usafirishaji wa umeme kutoka hapo kwenye uzalishaji kwenda kwenye gridi ya Taifa kituo cha kupokea na kupoza umeme eneo la Kidahwe sambamba na mradi wa kusambaza umeme kwa vijiji ambavyo umeme huo umepita kwenda kituo cha kupoza umeme.
 
Kwa sasa tayari miradi miwili imekamilika ambayo ni mradi wa kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka eneo la uzalishaji umeme kwenda eneo la Kupokea na kupoza umeme Kidahwe pia mradi wa kusambamba umeme umekamilika kwani upo umeme wa gridi kutoka kituo cha Kidahwe ambao umesafirishwa na kuja hapo kwenye mradi  na maeneo ya vijiji  saba vinavyoguswa na mradi huo ambapo kaya 5000 zimeunganishwa.

mwisho.



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3