Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
  MAREKANI WAPUNGUZA ONYO LA SAFARI KWA TANZANIA. YATHIBITISHA NI SALAMA.

MAREKANI WAPUNGUZA ONYO LA SAFARI KWA TANZANIA. YATHIBITISHA NI SALAMA.



Serikali ya Marekani imepunguza kiwango cha onyo kwa wasafiri wanaokuja Tanzania kutoka kiwango cha 3 (Fikiria Upya Safari) hadi kiwango cha 2 (Chukua Tahadhari), kuanzia tarehe 16 Oktoba 2026.


Hatua hii imekuja wakati sekta ya utalii nchini Tanzania ikirekodi mapato ya dola za Marekani bilioni 4.41 mwaka 2025.


Eneo ambalo wasafiri kutoka Marekani wameshauriwa kutokwenda ni mpaka wa Mtwara unaopakana na Msumbiji.


Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwa na fursa ya kuimarisha imani ya wageni, kukuza utalii na kupanua ushirikiano wa kimataifa.

Karibuni Tanzania ni salama.

#VisitTanzania #TanzaniaUSRelations #SamiaRaha

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3