Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
LUWALAJE KUANZA UTEKELEZAJI WA MIUNDOMBINU RAFIKI KWA WATU WENYE ULEMAVU

LUWALAJE KUANZA UTEKELEZAJI WA MIUNDOMBINU RAFIKI KWA WATU WENYE ULEMAVU

 


Na Matukio Daima Media, Chunya 


KATA ya Luwalaje, iliyopo katika Jimbo la Lupa wilayani Chunya, imeanza kuchukua hatua za kuboresha miundombinu ya shule za msingi ili kuwawezesha watoto wenye ulemavu kupata huduma ya elimu katika mazingira rafiki na jumuishi.


Diwani wa Kata hiyo, Leckson Mwakasuluka, amesema madarasa mengi yaliyojengwa miaka ya nyuma hayakuzingatia mahitaji ya watoto wenye ulemavu, hali iliyokuwa ikifanya baadhi yao kukabiliwa na changamoto ya kuyafikia madarasa na kushiriki kikamilifu katika masomo.


Akizungumza na mwandishi wa habari kuhusu mikakati ya kata hiyo katika kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wenye ulemavu, Mwakasuluka amesema wameanza kurekebisha baadhi ya madarasa ili yaweze kukidhi mahitaji ya kundi hilo.


Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata fursa sawa ya elimu kama watoto wengine, bila kukumbana na vikwazo vinavyotokana na miundombinu isiyozingatia mahitaji yao.


"Tumeendelea kurekebisha baadhi ya madarasa na kuyafanya yawe bora na ya kisasa ili yaendane na mahitaji ya kipindi cha sasa. Madarasa mengi yalijengwa zamani, wakati baadhi ya mahitaji muhimu hayakuzingatiwa, ikiwemo njia za kupandia kwa watu wenye ulemavu," amesema Mwakasuluka.


Ameongeza kuwa kwa sasa wanazingatia mahitaji ya makundi yote katika uboreshaji wa miundombinu, ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa fursa ya kupata elimu kutokana na changamoto za kimazingira.


Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuimarisha elimu jumuishi katika Kata ya Luwalaje.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3