DC KILINDI AHAIDI KUPAMBANA NA MIGOGORO YA ARDHI
Oct 27, 2026
*WANANCHI WATISHIA KUIBWAGA CCM
Na Danson Kaijage,Matukio Daima Media Kilindi.
MKUU wa Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga, Fauzia Ngatimbura,amesema kuwa kazi kubwa atakayo anza nayo katika Wilaya hiyo ni kupambana na migogoro ya ardhi ambayo imedumu kwa Muda Mrefu.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa malalamiko ya migogoro ya ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Kwekinkwembe na kutishia kuondoka CCM na kutimkia vyama vya upinzani.
Fauzia amesema kuwa licha ya kwamba ameingia ofisini siku ya jumatatu lakini atahakikisha anafanya kazi za wananchi kadri ya uwezo wake.
"Siwezi kuongerea zaidi juu ya migogoro ya ardhi kwa sasa ila najua kuwa migogoro hipo na kama unavyojua Mimi ndo nimeingia ofisini jumatatu tu ofisini.
"Naelewa kuwa ipo migogoro ya ardhi ambayo imetatuliwa na mingine imefiakia hatua fulami hivyo itabidi nipitie mafaili mbalimbali ili nione naanzia wapi hivyo nitaifanyia kazi migogoro hiyo ila kwa sasa siwezi kusema sana".ameeleza Fauzia.
Kabla Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Fauzia kutoa maelezo hayo wananchi wa Kijiji cha Kwekinkwembe kata ya Mkindi tarafa ya Mswati Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga, wametishia kurudisha kadi za uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa ardhi ambao hautatuliwi Kwa wakati.
Kutokana na hali hiyo wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati mgogoro wa ardhi baina ya Jamii ya Wakulima ya Wanguu na jamii ya wafugaji wa Kimasai.
Wananchi wametoa ombi hilo kwa Rais wakiwa wanaogea na waandishi wa habari juu ya hadha wanayokutana nayo kwa kufanyiwa uonevu na wafugaji wa jamii ya Kimasai.
Katika maelezo yao wameeleza kuwa kwa sasa wamejikita wakiishi maisha ya kukimbia kimbia huku na kule kutokana na kutishiwa na wafugaji hao huku wakieleza kuwa hata mashamba yao ya wanayokutumia kulima Kwa nia ya kujipatia kipato na vhakula yapo hatarini kuchukuliwa.
Mmoja wa wamemiliki wa shamba hayo ni Bakari Salimu Omari,Mkazi wa kijiji cha Kwekinkwembe ameeza kuwa jamii hiyo ya wakulima imeanza kumiliki mashamba hayo muda Mrefu.
Akiendelea kutoa ufafanizi alieleza kuwa kuwa kijiji Kwekinkwembe kilianzishwa mwaka 1971 na ilipofia mwaka 1976 kilinzishwa Kijiji cha Mkindi na kuwekeana mipaka.
Pamoja na mambo mengine Omari ameeleza kuwa tatizo kubwa au ombi kubwa la wananchi ni kutaka viongozi kuhakikisha wanatatua mgogoro huo ikiwa ni pamoja na kuweka mipaka ya maeneo.
Naye Lukuwa Kabwanga chanzo chote cha migogoro ni kuingiliwa na jamii ya wafugaji ambao ni jamii ya kimasai.
Kwa upande wake Halima Kilo alieleza kuwa kitendo cha kuingiliwa kwenye mashamba yao na jamii ya wafugaji kinachangia kwa kiasi kikubwa kuwakosesha mapato na ikiwa ni pamoja na watoto kutokwenda shule.
Kwa upande wa Mtendaji wa kata ya Mkindi aliyejitambilisha kwa jina moja la Makusudi alipotafutwa kuhusu mgogoro huo alisema kuwa mpaka Sasa Kuna mgogoro huo ambao ni wa siku nyingi lakini bado wanaendelea kusikiliza viongozi ambao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi ili aweze kutoa mwongozo.
Mwisho.


