Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 LP PADS KUWAFIKIA WANANCHI, MASANJA AULA

LP PADS KUWAFIKIA WANANCHI, MASANJA AULA


Matukio DaimaMedia 

Katika kuhakikisha huduma za kijamii zinasogezwa karibu na wananchi, Kampuni ya LP PAD Trading Co. Limited leo imezindua bidhaa mpya ya taulo za kike ambapo imelenga kuwafikia wanawake na wasichana.

Aidha, pia imejipanga kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kuendelea kutoa ajira kupitia shughuli zake za usambazaji, masoko na mauzo, huku ikisisitiza kuwa upatikanaji wa taulo bora za kike ni haki muhimu kwa kila mwanamke na msichana.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa LP PAD Trading Co. Limited, Martin Kadinda, amesema kampuni hiyo imekuja na dhamira ya kuhakikisha wanawake na wasichana wa Tanzania wanapata taulo za kike zenye ubora wa hali ya juu kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Kadinda amesema LP PADS ni bidhaa inayolenga kuchangia afya na usafi wa hedhi kwa wanawake na wasichana, huku kampuni hiyo ikijipanga kusambaza bidhaa zake katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwafikia walengwa wengi zaidi.

Aidha, imemtangaza msanii na mrembo maarufu nchini Tanzania Queen Masanja kuwa balozi mpya wa bidhaa hiyo, huku uteuzi huo umetokana na ushawishi mkubwa alionao kwa jamii.

Kwa upande wake, Queen Masanja amesema anafurahi kuaminiwa na LP PAD Trading Co. Limited na kupewa jukumu la kuwa balozi wa bidhaa hiyo, hivyo ameahidi kuitendea haki na kuhakikisha bidhaa hiyo inawafikia wadau wengi zaidi.

"Ninafuraha kuwa sehemu ya safari hii muhimu ya kuhamasisha afya, usafi na ustawi wa wanawake na wasichana wa Tanzania, ninaamini LP PADS zitasaidia wanawake wengi kupata taulo za kike bora kwa bei nafuu na kwa urahisi," amesema Queen Masanja.

Sambamba na uzinduzi huo, Martin Kadinda ametangaza fursa kwa mawakala wa biashara, wasambazaji na wafanyabiashara kutoka mikoa mbalimbali kushirikiana na kampuni hiyo katika kusambaza LP PADS nchini kote.

MWISHO

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3