MWENGE WA UHURU 2026 WAPOKELEWA MTAMA KUZINDUA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 5.4
Na Hadija Omary
Lindi.........Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 umepokelewa rasmi Wilaya ya Lindi halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi ukitokea Wilaya ya Ruangwa.
Hafla ya makabidhiano imefanyika Viwanja vya Kambi ya Wachina, Tarafa ya Mtama, Kata ya Nyangao, ikishuhudiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi. Victoria Mwanziva Amesema Katika halmashauri hiyo ya Mtama, Mwenge utakimbizwa kwenye Jimbo moja la Uchaguzi, Jimbo la Mtama, ukipitia Tarafa 2 na Kata 5 kwa umbali wa jumla ya kilometa 58.3.
Alisema Mwenge wa Uhuru utapitia miradi 5 yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 5,412,232,600 ambapo Kati ya hizo Mchanganuo wa fedha ni: Serikali Kuu Sh. 4,100,000,000 Mchango wa wahisani Sh. 1,204,410,000 Michango ya Halmashauri Sh. 105,326,000 Nguvu za wananchi Sh. 24,966,000
Kati ya miradi hiyo, 4 itawekewa jiwe la msingi na mmoja utazinduliwa. Miradi hiyo inahusu Sekta ya Afya, Elimu Awali na Msingi, Elimu Sekondari, Viwanda na Uwekezaji, pamoja na Maendeleo ya Jamii.
Kwa upande wake kiongozi wa wakimbiza mwenge Kitaifa 2026 Wazo Mwang'onda aliwataka wataalamu wote wanaohusika na Miradi hiyo itakayofikiwa na mwenge WA uhuru pamoja na vifaa husika viwepo Katika Eneo la Mradi sambamba na kuwepo kwa taarifa sahihi za Miradi husika
Mwishooo


