Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
DEREVA WA LORI ASIMULIA NJINSI ALIVYONUSURIKA KIFO,AJALI YA BASI LA SHABIBY NA LORI

DEREVA WA LORI ASIMULIA NJINSI ALIVYONUSURIKA KIFO,AJALI YA BASI LA SHABIBY NA LORI

 

MATUKIO DAIMA MEDIA.

IRINGA.Dereva wa Lori  aliyenusurika katika ajali ya basi la shabiby asubuh ya leo lililokuwa likitoka Dodoma kwenda Mbeya amesema kuwa hakuamini kama angeweza kutuliza Lori  analoendesha ili kudhuia maafa zaidi.

TAZAMA MAHOJIANO YA DEREVA BOFYA LINK HII

James alisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na lori  la kampuni ya pepsi kufeli break na kushindwa kusimamisha roli hilo na kukosa uelekeo na kwenda kuligonga uso kwa uso basi la abilia kampuni ya shabiby.

“Tuliona Lori  la peps limefeli break tangu umbali mrefu dereva akawa anahangaika kulisimamisha bila mafanikio na baada ya kushindwa kulimudu akaenda kuligonga basi la shabib uso kwa uso na kusababisha ajali ambayo imepelekea vifo pamoja na majeruhi”alisema 


Katika ajali hiyo watu watano wamefariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Shabiby lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mbeya na Roli la vinywaji kampuni ya peps.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba usiku, katika eneo la Tanangozi Mkoani Iringa ambapo majeruhi 17 wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa wakipatiwa matibabu.

Akizungumza na wanahabari Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Dkt Alfredy Mwakalebela alisema walipokea miili mitano ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo sambamba na majeruhi 28 ambao walipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.


 “Alfajili ya saa 11 tulipokea majeruhi ya ajali ya basi la shabiby na  Lori la vinywaji ambapo tulipokea maiti 5 na majeruhi 28 na wamepatiwa matibabu na mapaka sasa waliolazwa ni 17 huku kati yao watano wako mahututi na  wengine waliruhusiwa baada ya matibabu”Alisema Mwakalebela

Alisema kuwa kati ya hao 17 waliolazwa mmoja ni raia wa Asia ambaye ameumia vibaya maeneo ya kichwa na wanatarajia kumsafirisha kwenda hospitali ya Muhimbili kupatiwa matibabu zaidi.TAZAMA WALICHOSEMA MASHUHUDA BOFYA LINK HII

Wakizungumza baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa walipata taarifa za ajali majira ya saa 7 usiku na baade kufika katika hospitali ya rufaa kujua hali za wagonjwa na ndugu waliokuwa katika ajali hiyo.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3