Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MANGE KIMAMBI AFUNGULIWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

MANGE KIMAMBI AFUNGULIWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

 


Mange Kimambi, ambaye anaishi nchini Marekani, amefunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi nchini Tanzania.

Anakabiliwa na shtaka moja la utakatishaji fedha linalohusisha kiasi cha Sh milioni 138.5.

Kesi hiyo imepangwa kutajwa tarehe 4 Desemba mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Hassan Makube katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Shitaka hilo liliwasilishwa na upande wa mashtaka tarehe 28 Agosti mwaka huu.

Asubuhi ya tarehe 2 Desemba 2025, Mange alionekana katika video iliyosambaa kwa wingi mitandaoni akithibitisha kuwa amepewa taarifa za mashtaka hayo, akidai kuwa Serikali ya Tanzania inapanga kumrudisha nchini.

Katika Kesi ya Jinai Na. 000021172 ya 2025, kosa linalodaiwa linahusiana na Sheria ya Utakatishaji Fedha, ikisomwa pamoja na Sheria ya Kudhibiti Uhalifu wa Kiuchumi na Ugaidi.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, upande wa mashtaka unadai kuwa kati ya tarehe 1 Machi hadi 31 Machi 2022, katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, alijipatia Sh milioni 138.5 akijua kuwa fedha hizo zilikuwa mapato yatokanayo na uhalifu.

Aidha, inadaiwa kuwa Mange alizipata fedha hizo kwa kufanya kazi kama mwandishi wa habari bila uthibitisho (accreditation) na kwa kudai fedha hizo kwa vitisho.

HABARI NA NAFASI ZA AJIRA JIUNGE NA MATUKIO DAIMA APP LEO NI BURE KABISA BOFYA LINK HII CHINI ⬇️

JIUNGE NA APP YETU BONYEZA HAPA


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3