KIKUNDI CHA FRIENDS OF IRINGA CHAWAFARIJI WATOTO WENYE ULEMAVU NYUMBA ALLI
Baadhi ya wanawake wa kikundi cha Marafiki wa Iringa (Friends of Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa kikundi hicho Edward Mwita (wa sita kushoto mstari wa mbele) Mara banda ya kukabidhi Msaada kwa watoto wenye ulemavu wa kituo cha Nyumba Alli Wilolesi Iringa mjini (l
NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.
Kikundi cha umoja wa marafiki wa Iringa (Friends of Iringa)wametembelea na kutoa msaada wa vitu mbali mbali na pesa zaidi ya shilingi milioni 3 kwa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Nyumba Ali kilichopo Wilolesi mjini Iringa.
Marafiki hao wameguswa kutoa sadaka hiyo ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kutimiza miaka miwili tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho chenye lengo la kusaidiana katika shida na raha.
Akizungumza Muasisi wa umoja huo Edward Mwita wakati akisoma taarifa ya kukundi hicho walipotembelea taasisi ya nyumba ali alisema kuwa watu wenye ulemavu ni watu ambao wanahitaji kutimiza ndoto zao hivyo ni vyema kuwakumbuka kwa faraja na kuwapa mahitaji.
"Nje ya mahitaji ya chakula pia kama kikundi tumetoa fedha taslimu kwa ajili ya kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali ambayo sisi hatujafanikiwa kuyatimiza kwa siku ya leo"alisema Mwita
Akitoa taarifa ya kituo mmoja wa watumishi katika taasisi ya Nyumba Ali, Fuko Julias Paul alisema kuwa taasisi ya Nyumba Ali imejikita zaidi katika kulea na kuhudumia watoto wenye ulemavu.
Alisema kuwa taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2006 mpango ukiwa ni kuanzisha kituo cha kulea watoto wakike wenye ulemavu.
Fuko alisema kuwa changamoto walizonazo watoto wanaowahudumia zinaanzia kwenye ubongo na hakuna dawa u ubongo,hivyo watoto hao wanahitaji mazoezi tiba ili mtoto aweze kupata maendeleo.
"Ili apone inabidi autibu ubongo wake,na mapaka sasa hakuna dawa ya ubongo duniani, mbali na hufduma ya mazoezi bado tunahuduma ya elimu ambayo namna ya ufundishaji ni tofauti na watoto wa kawaida"alisema
"Kupitia mfumo wa elimu wamepata mafanikio makubwa kwa kuwasomesha watoto wenye ulemavu ambapo tuna watoto wa madarasa tofauti ambao wanasoma katika mfumo wetu wa elimu, mbali na elimu tuna karakana ambapo tunawafundisha stadi za maisha, tuna nyumba shuku(Hostel) ambayo inatumika kuwalea watoto wanaoishi katika mazingira magumu"alisema.
Mwenyekiti wa wazazi ambaye pia ni afisa uhusiano katika taasisi hiyo Zawadi Msigala alisema kuwa yeye ni mlemavu ambaye ameishi miaka 27 na ulemavu huo.
Alisema kuwa anafurahia kuwa mlemavu kwa kuwa ulemavu wake umempa fursa kubwa ya kutambulika na kufanya vitu vingi.
Aidha alisema kuwa labda asingekuwa mlemavu angekuwa miongoni mwa vijana wanaovuta bangi mtaani au vijana wanaodai haki na hawajui ni haki gani wanadai.
"Kwa kuwa ni mlemavu nimepata firsa ya kufanya vitu vingi kwa sababu tu ni mlemavu,taasisi ya nyumba ali inapokea misaada mingi kutoka ulaya lakini sisi walemavu sio wazungu hatujazaliwa ulaya ni watoto wa hapa Tanzania"
"Ombi langu sisi wenyewe watanzania tuendelee kusapoti watoto walemavu kwa sababu watoto hao pia wanahitaji malezi na mahitaji muhimu kama shule na malezi ili waweze kujiendeleza na kutimiza ndoto zao, kwa kuwa kuwa na ulemavu ni baraka kutoka kwa Mungu na sio laana"alisema Zawadi
Aidha Zawadi alisema kuwa endapo wazazi watapata mtoto mwenye ulemavu wasiwafungie ndani wala wasiwatenge kwa sababu yeye anaamini ulemavu ni zawadi kutoka kwa Mungu.
mwisho.

