MWENGE WA UHURU WAANZA RASMI ZIARA YA SIKU 9 MORO,MIRADI 63 YA ZAIDI YA BILION 50 KUKAGULIWA.
Matukio Daima,Morogoro
Mkoa wa Morogoro umeanza rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru baada ya kupokea mwenge huo katika hafla iliyofanyika wilayani Gairo.
Makabidhiano hayo yalifanywa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, aliyemkabidhi mwenge huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima.
Katika kipindi cha siku tisa ambazo Mwenge wa Uhuru utakaa mkoani hapa, unatarajiwa kutembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuzindua miradi iliyokamilika pamoja na kuweka mawe ya msingi kwa miradi mipya.
Jumla ya miradi 63 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 50 itafikiwa na Mwenge wa Uhuru katika halmashauri mbalimbali za mkoa huo.
Ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu wa kitaifa wa kuhamasisha maendeleo, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali za umma kupitia miradi inayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi.



.jpeg)







